Familia ya Patrice Lumumba yapambana kutafuta haki Ubelgiji
21 Januari 2026
Matangazo
Familia ya aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa Kongo Huru, Patrice Lumumba, imesema ina matumaini ya kupata haki kufuatia hatua ya Mahakama ya Ubelgiji kufikiria kumfungulia mashtaka mshukiwa pekee aliyebakia wa mauaji ya kiongozi huyo mnamo mwaka 1961.
Genge la wahalifu lavamia makumbuyho ya kaburi la Lumumba DRC
Kwa miaka 15 iliyopita familia ya Lumumba imekuwa ikishinikiza kufanyika kile inachosema, haki ya kisheria dhidi ya maafisa wa Ubelgiji waliohusika kwenye mauaji ya mwanasiasa huyo maarufu.
Etienne Davignonmwenye umri wa miaka 93, aliyewahi wakati mmoja kuwa kamishna wa Umoja wa Ulaya alikuwa mwanadiplomasia wa Ubelgiji wakati wa mauaji ya Lumumba yaliyofanywa miaka 65 iliyopita na mamluki kutoka Ubelgiji.