1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachimbaji madini Afrika Kusini bado wakwama chini

Sylvia Mwehozi
16 Novemba 2024

Jamaa waliokata tamaa wa mamia ya wachimba madini haramu waliokwama chini ya ardhi kwenye shimo lisilotumika la mgodi nchini Afrika Kusini, wameendelea kusubiri kwa matumaini juu ya hatma ya wapendwa wao.

Shimo la kuingia mgodi uliotelekezwa Afrika Kusini
Shimo la kuingia mgodi uliotelekezwa Afrika KusiniPicha: AP Photo/picture alliance

Jamaa waliokata tamaa wa mamia ya wachimba madini haramu waliokwama chini ya ardhi kwenye shimo lisilotumika la mgodi nchini Afrika Kusini, wameendelea kusubiri kwa matumaini juu ya hatma ya wapendwa wao.

Wachimbaji hao wamo katika mvutano na polisi, ambao wamezuia vifaa vyao vya chakula na maji ili kuwalazimisha kutoka nje na kuwakamata kwa kuingia kinyume cha sheria katika mgodi uliotelekezwa kutafuta mabaki ya dhahabu.

Soma: Wachimba mgodi 955 waliokwama Afrika Kusini waokolewa

Waziri anayehusika na Polisi Senzo Mchunu, ambaye alitembelea eneo la mkasa siku ya Ijumaa, alisema kuwa mamlaka zitafanya kazi pamoja kuwatoa wachimbaji chini.

Wachimbaji hao wamekuwa chini ya ardhi kwa takriban wiki nne tangu polisi ilipozingira njia za kuelekea kwenye mgodi huo uliopo katika mji wa Stilfonteinkatika mkoa wa Kaskazini Magharibi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW