1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiKenya

Familia za wahanga janga la Solai Kenya wapata fidia

Wakio Mbogo28 Novemba 2023

Hatimaye familia za watu 48 walioangamia katika mkasa wa bwawa la Solai uliotokea mjini Nakuru, Kenya, mwaka 2018 wamepata fidia baada ya makubaliano na mshtakiwa mkuu.

Jengo la Mahakama ya Juu Kenya
Jengo la Mahakama ya Juu KenyaPicha: John Ochieng/SOPA Images/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Mahakama ilikubali ombi la kutatua kesi hiyo nje ya mahakama baada ya mshtakiwa kutoa shilingi milioni 73 za Kenya kama fidia.

Watu 48 baadhi yao wakiwa watoto walifariki kwenye mkasa huo, na zaidi ya familia 200 zikiachwa bila makao.

Perry Mansukh mmiliki wa bwawa hilo alikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji ya watu 48.

Watu wengine saba walishtakiwa wakiwemo maafisa wa serikali waliolaumiwa kwa kutotathmini ubora wa bwawa hilo kabla ya kutoa leseni na kuidhinisha itumiwe.

Wengi wa watu waliokuwa wakiishikaribu na bwawa la Solai ambao waliathirika, walikuwa wameajiriwa kwenye shamba la Perry Mansukh.

Familia zilizoathirika zimekubaliana kuwa kila mtu mzima aliyeathirika atalipwa shilingi milioni 1.2, na kila mtoto atalipwa shilingi laki nane.

Maafa kutokana na mvua Kenya

01:42

This browser does not support the video element.

Soma pia:Rais Ruto atangaza mikakati ya kukabiliana na mafuriko

John Ngugi alimpoteza mke wake kwenye mkasa huo amesema maisha yamebadilika tofauti na awali na wamepoteza vingi vikubwa katika msaka.

"Wakati ule nilikuwa na duka, nyumba na kioa kitu kilibebwa," Alisema.

Aliendelea kusema kwamba kulikuwa hakuna haja yakuendelea kumshikilia mmiliki wa bwawa hilo, kutokana na ukweli kwamba hakuna msaada wowote wanaoupata.

"pesa zote zilizochangwa na misaada iliotolewa kwa ajili yetu hatukupata chochote." Aliiambia DW kiswahili.

Julia Mawachi aliwapoteza watoto wawili kwenye mkasa huo wa tarehe 9 mwezi Mei mwaka 2018 bwawa la Solai lilipovunja kingo zake nakuwazomba watu, mifugo, nyumba, mali na mashamba.

Alisema hakuna kinachoweza kuyaondoa makovu aliyobaki nayo, ila ameridhika kuwa haki imetendeka na anapata fursa nyingine ya kuyaanza maisha yake upya.

Shinikizo la mashirika ya haki za binadamu

Uamuzi huu unakamilisha safari ya miaka mitano ambayo ilihusisha ushawishi mkubwa wa mashirika ya kiraia kama tume ya Kenya ya kutetea haki za kibinadamu KHRC na kamati ya sheria ya bunge la seneti.

Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu nchini Kenya Martha KoomePicha: John Ochieng/SOPA Images/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Mwezi Februari mwaka 2020 mahakama ya juu iliagiza washukiwawaachiliwe ikiamuru kuwa hawakuwa na kesi ya kujibu lakini waathiriwa wakarejelea mahakamani na kesi yenyewe ikafufuliwa tena Aprili mwaka huu.

Maafikiano haya mapya yamepelekewa kuondolowa rasmi kwa kesi hiyo ili fidia iweze kutolewa.

Soma pia:Mahakama Kenya yaamuru Mackenzie kubakia rumande

Perry Mansoukh mmiliki wa bwawa la Solai ambaye pia ndiye mshukiwa mkuu ameahidi ushirikiano mwema na jamii hiyo.

Zoezi hilo limetekelezwa wazi mbele ya wahusika na maafisa wa serikali wamedhibitisha kuwa fidia imezifikia familia zilizoathirika.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW