1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKimataifa

FAO: Bei ya vyakula duniani ilishuka mnamo mwaka 2023

5 Januari 2024

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema kuwa bei ya chakula duniani ilishuka mwaka 2023, huku wasiwasi ukipungua juu ya usafirishaji wa nafaka na mafuta.

Mazao ya nafaka
Nafaka ni moja ya mazao ya kile yanayotumika sana duniani kwa chakulaPicha: Benefit-Sharing Fund BSF/FAO

Shirika hilo lenye makao makuu yake mjini Rome Italia limeeleza kuwa, bei ya bidhaa za chakula duniani ilishuka kwa asilimia 13.7 mwaka 2023 ikilinganishwa na mwaka 2022.

Hata hivyo, bei ya sukari tofauti na bidhaa nyengine, ilipanda kwa asilimia 26.7 mwaka jana japo ilishuka tena mwezi Disemba hasa baada ya Brazil kuongeza usafirishaji wa mauzo yake ya nje.

Faharasa ya bei ya chakula ya FAO hufuatilia bei za soko la kimataifa za vyakula vikuu vitano vinavyotumika zaidi duniani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW