1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Faye aombwa kuzungumza na Mali, Niger na Burkina Faso

8 Julai 2024

Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, imemtaka rais wa Senegal Basirou Diomaye Faye kufanya mazungumzo na Mali, Niger na Burkina Faso, kufuatia uamuzi wa nchi hizo kujiondoa kwenye jumuiya hiyo

Bassirou Diomaye Faye hält seine Ansprache als senegalesischer Präsident
Picha: John Wessels/AFP

Watika wa mkutano wake wa kilele katika mji mkuu wa Nigeria Abuja, jumuiya hiyo ya ECOWASilimteuwa Faye kama mjumbe wake kukutana na viongozi wa nchi hizo tatu ambazo ziliunda muungano wao tofauti baada ya mapinduzi katika nchi zao kuharibu mahusiano na mataifa jirani.

Masharti ya mazungumzo hayo hayakubainishwa mara moja.

Soma pia;Mkutano wa ECOWAS wafanyika Abuja kutatua changamoto za kikanda

Wakati wa mkutano huo, Rais wa Tume ya ECOWAS Omar Alieu Touray, alisema kuwa rais huyo wa Senegal ambaye ni kiongozi mdogo zaidi barani Afrika baada ya ushindi wake wa uchaguzi mwezi Machi, ana sifa zote zinazohitajika kusimamia mazungumzo hayo.

Mali, Niger na Burkina Faso, zathibitisha kujiondoa kutoka ECOWAS

Siku ya Jumamosi, Mali, Niger na Burkina Faso, zilithibitisha kujiondoa katika Jumuiya hiyo katika mkutano wao wa kilele uliofanyika mjini Niamey nchini Niger.