FBI yapekua chuo kikuu Delaware kuchunguzi nyaraka za Biden
16 Februari 2023Upekuzi huo ulioripotiwa kwa mara ya kwanza na kituo cha utangazaji cha CNN, ulithibitishwa na mtu anaefahamu suala hilo aliezungumzwa kwa sharti la kutotajwa jina, na hakusema iwapo kuna chochote kilichopatikana.
Soma pia:Biden kuchunguzwa baada ya kukutwa na nyaraka za siri
Chuo Kikuu hicho ndiko alikosoma Biden, na mnamo mwaka 2011, alikipatia rekodi zake za miaka 36 ya uhudumu katika Baraza la Seneti. Rekodi za Seneti za Biden hazizingatiwi na sheria ya rekodi za rais, ingawa marufuku ya kushughulikia vibaya taarifa za siri bado inatumika.
Chuo hicho ndiyo taasisi ya nne inayojulikana ambako FBI imefanya upekuzi kufuatia ukaguzi wa ofisi yake ya zamani katika kituo cha Pen Biden, ambako nyaraza zenye alama za siri zilikutwa kwenye kabati lililofungwa na wanasheria wa Biden mwezi Novemba, na hivi karibuni zaidi katika nyumba zake za Delaware.