Wawakilishi wa Afrika Urusi 2018 kupokea mamilioni
1 Mei 2018Misri, Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia, zimefaulu kushiriki katika michuano y akombe la dunia itakayofanyika nchini Urusi, na rais wa shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad, alismea katika taarifa kwamba fedha hizo zitatumika "kushughulikia mapema, suala la bonasi za wachezaji."
Migogoro juu ya malipo katika michuano iliyopita, "ilipelekea kuwepo na hali zilizoathiri vibaya taswira ya soka barani Afrika, ikiwa kwa kiwango kikubwa utendaji wa timu viwanjani," aliongeza.
Mwaka uliopita, shirikisho la kandanda la Nigeria (NFF) lilisaini makubaliano na wachezaji wake wakiahidi kujiepusha na migogoro ya bonasi na malipo ambayo imeharibu kampeni zao za nyuma za kombe la dunia.
Wachezaji wa timu ya Nigeria, Super Eagles walihusika katika mzozo wa muda mrefu kuelekea mashindano ya kombe la shirikisho la mwaka 2013 nchini Brazil, na mgogoro juu ya bonasi pia ukavuruga kampeni yao ya kombe la dunia mwaka 2014.
Matatizo sawa na hayo yameziathiri timu nyingine na bara la Afrika.
Time 32 zinashiriki katika michuano ya kombe la dunia inayofanyika kuanzia Juni hadi Julai, hupokea kitita cha dola milioni 1.5 kila mmoja kutoka FIFA katika mfumo wa malipo ya maandalizi, na zinahakikishiwa kingine kisichopungua dola milioni 8 katika fedha za zawaidi baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.
Mwandishi: Iddi Ssessanga/rtre
Mhariri. Mohammed Khelef