1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA NA KOMBE LIJALO LA DUNIA. TIMU ZA TAIFA ZAPAMBANA KUANIA TIKETI ZA KOMBE LIJALO LA DUNIA 2006 UJERUMANI:

Ramadhan Ali7 Oktoba 2004

FIFA imearifu kwamba itazingatia kudai mashindano yote ya ligi za nyumbani yakamilishwe siku 25 kabla ya kuanza kwa Kombe lijalo la dunia 2006 litakaloaniwa Ujerumani.hii ni kuwapa wachezaji alao siku 8 za mapumziko na nyengine 17 za mazowezi na timu zao za taifa kabla mpambano wa kwanza katika Kombe hilo la dunia.

Kombe lijalo la dunia litaanza Juni 9,mwaka 2006 mjini Munich na Gelsenkirchen.Hii maana yake ,mashjirikisho ya dimba ya kitaifa yatabidi kumaliza mashindano ya ligi zao na vikombe vya Taifa hadi Mei 14.Halmashauri-tendaji ya FIFA inatumai kuidhinisha mwongozo huo wakati wa kikao chake cha desemba 18.

Ikikutana katika makao makuu yake mjini Zurich,Uswisi kati ya wiki hii, Halmashauri-tendaji ya FIFA iliamua kuongeza kipato cha timu 32 zitakazoshiriki katika kombe lijalo la dunia.Kitita cha faranga za Uswisi milioni 332 na kila timu kwa kushiriki tu hapa Ujerumani itajipatia ruzuku ya dala milioni 8.21.Huu ni muongezeko wa 38% kutoka malipo kila timu iliopata katika Kombe lililopita la dunia huko Korea ya kusini na Japan.

Katika medani ya dimba, FIFA iliamua pia mabingwa wa Kombe la mashirikisho kutoka Ulaya na Amerika Kusini sio lazima zishiriki katika Kombe la mashirikisho ambalo linalofuata litachezwa hapa Ujerumani,Juni mwakani kufungua pazia kwa kombe la dunia mwaka mmoja baadae.

Halkadhalika FIFA imeamua kwamba baada ya Kombe la dunia la wanawake 2007,mashindano hayo 2 ya Kombe la dunia-wanawake na wanaume yachjezwe mwaka ule ule mmoja na hii itakua kuanzia 2010,mwaka ambao Kombe la dunia kwa mara ya kwanza litaaniwa Afrika-Afrika kusini.Hatua hii shabaha yake ni kutoa mapumziko ya miaka 2 kati ya michezo ya olimpik na Kombe la dunia la wanawake.

Katika hatua zake nyengine ilizotangaza kati ya wiki hii,FIFA imesimamisha uwanachama wa shirikisho la dimba la Niger kutokana na kujiingiza serikali katika shughuli zake za dimba.Kusimamishwa kwa Niger kulikoanza wiki hii mara moja, hakutaathiri lakini changamoto za mwishoni mwa wiki hii kanda ya Afrika kuania tiketi za kombe lijalo la dunia kwavile, Niger imeshapigwa kumbo.Nigeri ilitolewa na Algeria.

FIFA pia imeiambia Ethiopia na Nigeria kutatua mivutano yao ya ndani ya nchi.Juni 2, utakumbuka kuwa FIFA ilisimamisha uanachama wa Kenya kwa kujiingiza pia kwa serikali zao katika shughuli za chama cha mpira cha nchi hiyo.Marufuku hayo sasa yameondolewa na leo Kenya imerudi tena uwanjani kupambana na Botswana kuania tiketi yake ya Kombe la dunia.

FIFA pia iliamua wiki hii kuwa kwa mara ya kwanza katika historia yake, mkutano mkuu wa FIFA-Congress-ufanyike barani Afrika.Mji wa Marrakesh wa Morocco, umechaguliwa kituo cha mkutano huu mwaka ujao,ambapo chama cha mpira cha Morocco kitaadhimisha mwaka wake wa 50 tangu kuasisiwa.

FIFA imetangaza orodha ya timu bora ulimwenguni wakati huu na inaongozwa na mabingwa wa dunia Brazil,wakifuatwa na Ufaransa huku Argentina ikichupa hadi nafasi ya 3.

Spain inafuata nafasi ya 4 huku Holland ikisimama nafasi ya 5.jamhuri ya czech inafuata nafasi ya 6 huku Uingereza na Ureno zikija nafasi ya 7 na ya 8.Ujerumani imeangukia nafasi ya 13 nyuma ya Uturuki.Katika orodha hii timu pekee ya Afrika ni Nigeriaikiwa nafasi ya 18.Iran inayocheza na Ujerumani hivi punde ,iko nafasi ya mwisho ile ya 20 katika orodha ya FIFA.

Orodha ya FIFA kwa bara la Afrika imeiweka kileleni pia Nigeria,ikifuatwa na Kamerun –simba wa nyika na Misri ikiangukia nafasi ya 3.Senegal iliotia fora katika Kombe lililopita la dunia iko ngazi ya 4 ikifuatwa na Morocco huku mabingwa wa Afrika Tunesia nafasi ya 6.Bafana bafana-Afrika Kusini wako nafasi ya 7.Wakati Kenya iko nafasi ya 19, Rwanda imeangukia nafasi ya 22 ikifuatwa na jirani Uganda .Tanzania iko nafasi ya 45 na Djibouti inaburura mkia.

Mwishoni mwa wiki hii,timu kadhaa za dunia zimeingia uwanjani kwa changamoto za kuania tiketi za Kombe lijalo la dunia:Katika kanda ya Afrika,simba wa nyika-kamerun wanapambana na Sudan mjini Khartoum,Rwanda ina miadi na Algeria na Nigeria imewasili Libreville kuchuana na Gabon lakini bila ya mastadi wake wengi walioumia:Mpya kati ya hao ni Garba Lawal anaecheza Ureno n a hatakua uwanjani jumamosi.Nigeria tayari inawakosa akina J-J.Okocha na mshambulizi Julius Aghahowa.

Katika changamoto nyengine za kukata tiketi za Kombe lijalo la dunia mwishoni mwa wiki hii:Uganda yaumana na Bafana Bafana-afrika Kusini,Ghana ina miadi na simba wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.benin inakutana na vishindo vya Tembo wa Ivory Coast.Angola yaumana na Zimbabwe wakati Guinea mahasimu wao ni Morocco.

Mshambulizi hatari kabisa wakati huu,mholanzi Roy Makaay,ametangaza kati ya wiki hii nia yake ya kubakia na Bayern Munich, mabingwa mara kadhaa wa Ujerumani hadi mwisho wa maisha yake ya dimba la kuajiriwa.Makaay amedai aweza bado kutamba hadi kufikia umri wa miaka 35. Akiwa na umri wa miaka 29 hivi sasa,Makaay ameshatia mabao 40 katika mapambano 53 tangu kujiunga na Bayern Munich msimu uliopita kutoka klabu yake ya Spain ya Deportivo la Coruna.

Nae msghambulizi wa Brazil,Ailton,aliongoza orodha ya watiaji magoli katika Bundesliga-ligi ya Ujerumani msimu uliopita,ameungama kwamba klabu fulani katika Ligi ya Japan inamtaka ajiunge nayo kwa kitita kikubwa cha fedha.Ailton amesema anazingatia kuhamia Japan.Wakati huu laikini, Ailtonana mkataba na klabu ya Ligi ya Ujerumani Schalke .

Ailton,alijiunga na schalke msimu huu kutoka klabu bingwa Werder Bremen, lakini hadi sasa hakunawiri kama vile alivyonawiri msimu uliopita alipoichezea klabu bingwa Bremen.Ailton akitazamiwa kurudi Ujerumani kutoka nyumbani Brazil hivi karibuni,schalke ikitumai kwamba, atakua amechangamka na kurudi tena kutia mabao ka ma msimu uliopita.wakati huu ni Mjerumani wa asili ya Ghana,gerald Asamoah anaetia mabao kwa Schalke akishirikiana na Mdenmark Ebbe Sand.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW