1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA: Nusu ya watu duniani waliangalia kombe la dunia 2018

Sekione Kitojo
21 Desemba 2018

Zaidi  ya  watu  bilioni 3.5 waliangalia  fainali za  kombe  la  dunia katikati  ya  mwaka  huu  nchini  Urusi, kwa  mujibu wa  shirikisho  la kandanda  duniani FIFA.

FIFA Fußball-WM 2018 | Kroatien Vize-Weltmeister | Fans in Zagreb
Mashabiki wa timu ya taifa ya Croatia katika mchezo wa fainali dhidi ya Ufaransa 2018Picha: Reuters/M. Djurica

FIFA imesema uhakiki uliofanywa  na kampuni ya  Publicis Media Sport and Intertainment of World Cup utazamaji  ulionesha  kwamba watu  bilioni 3.572 waliatazama  kakriban  baadhi  ya matukio  ya mashindano  hayo  kuanzia  Juni 14  hadi  Julai 15 katika  televisheni nyumbani kwao, katika  majukwaa  ya  kidigitali, maeneo  ya  wazi ya  umma ama  katika  mabaa  na  mikahawa.

Mashabiki wa timu ya taifa ya Ufaransa wakishangiria mitaani baada ya timu yao ya taifa kunyakua taji la dunia 2018 nchini UrusiPicha: Reuters/G. Fuentes

Ripoti hiyo  inasema  tarakimu  hizo  zinawakilisha  asilimia  51.3 ya watu  wote  duniani  wenye  umri  wa  miaka  kuanzia  minne   na zaidi. Fainali  kati ya  Ufaransa  na  Croatia  ilishuhudia  watu  bilioni 1.2 wakiangalia  kwa  takriban hata  dakika  moja  tu.

FIFA imesema  ripoti hiyo inaonesha  kwamba  kwa  muda wa utazamaji  wa  wastani  umepanda  ikilinganishwa  na  fainali  za kombe  la  dunia  zilizofanyika  nchini  Brazil mwaka  2014, ambapo watu bilioni 2.49  walitazama  mashindano  hayo  kwa  takriban dakika  30, ikiwa  ni  juu  kutoka  watu  bilioni 1.95 miaka  minne iliyopita.

Djibril Sidibe mchezaji wa Ufaransa akifurahia kunyakua taji la ubingwa wa dunia 2018Picha: picture-alliance/ATP/A. Jamali

Wastani  wa  kati  wa  utazamaji  kwa  kila  mchezo  kati  ya michezo  64 ilikuwa  watu  milioni 191, ikiwa  ni  ongezeko  kutoka watu milioni 187 mwaka  2014  nchini  Brazil, FIFA  limesema , "kila mchezo  ulikuwa  ni  tukio la  televisheni  duniani  katika  kiwango chake."

Watazamaji wakiangalia mchezo wa fainali katika eneo la wazi nchini UfaransaPicha: Reuters/C. Platiau

Lakini  watu  walioshuhudia  mchezo  moja  kwa  moja  kwa  ajili  ya fainali  ilishuka  kwa  asilimia  5.1 na ule  wa  nusu  fainali  ulipukuwa chini  ya  asilimia  15.5 kuliko  mwaka  2014  ambapo uhakiki umesema  kwamba  sababu  ni  pamoja  na uchache  wa  idadi  ya watu  katika  nchi zilizohusika  na  ni  shirikisho  moja  tu lililowakilishwa , yaani  shirikisho  la  kandanda  barani  Ulaya  UEFA katika  timu  nne  za  nusu  fainali  katika  fainali  hizo  za  Urusi. Awamu  ya  makundi  na  timu  bora  zilizoingia  katika  awamu  ya timu  16 utazamaji  ulipanda  kwa  ulinganisho.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / dpae