1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoZambia

FIFA yachunguza unyanyasaji kijinsia timu ya Zambia

4 Agosti 2023

Shirikisho la soka duniani FIFA linachunguza malalamiko ya utovu wa nidhamu yanayohusiana na timu ya wanawake ya Zambia.

FIFA Frauen Fußball WM Sambia Costa Rica Barbra Banda
Picha: Juan Mendez/AP Photo/picture alliance

Kwenye kombe la dunia la wanawake, na kuapa kutoa adhabu kali ikiwa itathibitishwa.

Ingawa FIFA haikutoa maelezo ya kina, lakini ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa malalamiko hayo yanahusiana na tukio la kocha Bruce Mwape kudaiwa kumshika matiti mchezaji.

Soma pia: Kombe la Dunia: Afrika Kusini na Zambia zapokea kichapo

Madai ya unyanyasaji wa kijinsia katika timu ya wanawake ya Zambia yalienea kwenye mitandao ya kijamii mnamo mwaka jana na kuzuka tena mwaka huu wakati wa kombe la dunia huku kocha Mwape akiandamwa na maswali mengi.

Zambia ilitolewa katika hatua ya makundi ya michuano hiyo nchini Australia na New Zealand baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Uhispania na Japan kabla ya kushinda mechi yake na Costa Rica.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW