1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA yaitaka Iran kutimiza ratiba ya Kombe la Dunia

Josephat Charo
20 Machi 2026

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA linaitaka Iran ikamilishe ratiba ya michuano ya kombe la dunia la kandanda. Haya ni kwa mujibu wa kauli ya rais wa FIFA Gianni Infantino

Rais wa FIFA Gianni Infantino amesema Iran lazima ifuate ratiba ya kombe la dunia la kandanda 2026
Rais wa FIFA Gianni Infantino amesema Iran lazima ifuate ratiba ya kombe la dunia la kandanda 2026Picha: Jia Haocheng/REUTERS

Katika taarifa iliyotolewa jana Alhamisi ambayo hakuitaja moja kwa moja Iran, rais wa FIFA Gianni Infantino alisema soka ina jukumu muhimu katika kukuza amani, ingawa shirikisho hilo halikuchukua hatua yoyote kuhusu malalamiko ya mwanachama wake shirikisho la soka la Palestina dhidi ya Israeli.

Infantino alisisitiza baada ya baraza la utawala la FIFA kukutana kwamba halitakubali maombi ya Iran ya kuhamisha michezo mitatu ya makundi ya kombe la dunia ya timu hiyo mwezi Juni kutoka Marekani hadi Mexico.

Serikali ya Iran na maafisa wa soka wamesema haiwezekani kwa timu ya taifa kuja Marekani kutokana na mashambulizi ya kijeshi nchini humo kutoka kwa Israeli na Marekani tangu Februari 28. Timu hiyo inatarajiwa kucheza michezo miwili katika uwanja wa Los Angeles Rams huko Inglewood na mmoja huko Seattle.

FIFA pia iliamua Alhamisi kutochukua hatua yoyote kuhusu malalamiko rasmi ya shirikisho la soka la Palestina mwaka 2024 dhidi ya shirikisho la soka la Israeli, ikiwa ni pamoja na kusimamisha uanachama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW