FIFA yamfungia mwamuzi wa Tanzania
27 Februari 2019Shirikisho la kandanda duniani FIFA limesema kamati yake ya maadili imeweka marufuku ya maisha dhidi ya mwamuzi Oden Charles Mbaga kutoka Tanzania kwa kupokea hongo. Shirikisho la FIFA limesema Mbaga pia amepigwa faini ya dola laki mbili.
Haijafahamika wazi ni vipi FIFA inaweza kutekeleza faini hiyo kwa ajili ya tabia ambayo ni kinyume na maadili. Bila ya kutoa maelezo ya rushwa, FIFA imesema Mbaga alikiuka sheria ya mwaka 2009 ya maadili licha ya kuwa uchunguzi ulianzishwa mwezi Julai mwaka jana.
Mbaga anaripotiwa kuhusika na mtu anayetuhumiwa kupanga matokeo Wilson Perumal wa Singapore, ambaye amehusika katika kuwapata waamuzi katika michezo ya kirafiki katika utabiri wa matokeo bandia.