1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA yamsimamisha kazi Luis Rubiales kwa siku 90

26 Agosti 2023

Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka duniani FIFA imemsimamisha kwa muda wa siku tisini Rais wa shirikisho la soka la Uhispania Luis Rubiales.

FIFA Fußball Frauen-WM | Luis Rubiales küsst Jennifer Hermoso
Picha: Noe Llamas/Sport Press Photo/ZUMA Press/picture alliance

Katika kipindi hicho Rubiales hatoruhusiwa kujihusisha na shughuli zozote zinazohusiana na mpira wa miguu. 

FIFA iliagiza pia Rubiales na shirikisho la soka la Uhispania kuepuka kujaribu au kufanya mawasiliano ya aina yoyote na mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake Jennifer Hermoso. 

FIFA kufungua kesi dhidi ya rais wa shirikisho la soka la Uhispania

Rubiales aliibua hasira miongoni mwa watu baada ya kumbusu Hermoso mdomoni baada ya timu ya taifa ya Uhispania kuibuka washindi wa kombe la dunia la wanawake hivi karibuni.

Alikataa kujiuzulu na kusema kuwa Hermoso aliridhia kitendo hicho, madai ambayo Hermoso ameyakanusha
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW