1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA yatoa maagizo mapya kwa Urusi

28 Februari 2022

Shirikisho la kabumbu ulimwenguni FIFA lilijibu shinikizo la kimataifa linaloongezeka kuhusiana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine likisema Urusi itacheza mechi zake za nyumbani katika viwanja visivyoegemea upande wowote

Fedor Smolov Fußball Nationalmannschaft Russland
Picha: Alexander Kulebyakin/Russian Look/imago images

Shirikisho la kabumbu ulimwenguni FIFA jana lilijibu shinikizo la kimataifa linaloongezeka kuhusiana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine likisema Urusi itacheza mechi zake za nyumbani katika viwanja visivyoegemea upande wowote. FIFA pia imezuia wimbo wa taifa na bendera za Urusi kupeperushwa kwenye mechi hizo.

FIFA imesema kwenye taarifa yake kwamba itaendeleza majadiliano na kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC, shirikisho la soka barani Ulaya UEFA na mashirika mengine ya michezo ili kuangazia hatua yoyote zaidi ama vikwazo ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kutengwa kwenye michuano hiyo iwapo hali haitaimarika haraka.

Tangazo hilo linatolewa wakati mataifa hayo mawili yakiwa yamefuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia mwakani huku Ufaransa na Uingereza, Sweden Jamhuri ya watu wa Czech yakisema hayatacheza na Urusi.

afp

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW