1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FINALI YA KOMBE LA CONFEDERATIONS CUP JUMATANO NI KATI YA BRAZIL NA ARGENTINA

27 Juni 2005

Katika Kombe la mashirikisho-Confederations Cup, Argentina jana iliitoa Mexico kwa mabao 6-5 kwenye changamoto za mikwaju ya penalty na imekata tiketi ya finali ya kombe hilo keshokutwa mjini Frankfurt kati yake naBrazil.Kabla ya changamoto hiyo ya mikwaju ya penalty, timu hizo mbili zilisimama sare bao 1:1.

Carlos Salcido aliipatia Mexico bao mnamo mdakika ya 104 ya mchezo na kila mmoja akidhani Argentina imetolewa, Luciano Figueroa alisawazisha dakika 6 baadae.Tangu Argentina hata Mexico zilimaliza mechi ya jana zikiwa na wachezaji 10 –mmoja kutoka kila timu alitimuliwa nje na rifu kwa ngware.

Upande wa Argentina hatima hiyo ilimkumba Javier Saviola mnamo dakika ya 90 ya mchezo.Rafael Marquez wa Mexico akamfuata nje ya chaki ya uwanja.Wakwa wachezaji wa kwanza katika mapambano 14 kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika Kombe hili.

Argentina inafunga sasa safari kutoka Hannover kwenda mjini Frankfurt kwa miadi keshokutwa jumatano na mabingwa wa dunia Brazil marudio ya changamoto yao ya wiki 2 nyuma pale Argentina ilipoichezesha Brazil mjini Buenos Aires na kuizaba 3:1.Brazil itapania kulipiza kisasi .

Ujerumani lakini ilishindwa kulipiza kisasi na Brazil ilipozabwa mabao 3:2 hapo jumamosi na kesho itarudi uwanjani kukutana na Mexico mjini Leipzig kkunyan’ganyia nafasi ya 3 nyuma ya Brazil na Argentina.

Ujerumani nayo ilitaka kulipiza kisasi hapo jumamosi kwa kupokonywa Kombe na Brazil katika finali ya Kombe la dunia 2002 huko Japan.Mwishoe lakini,Brazil iliitoa Ujerumani kwa mabao 3:2.

Ulikuwa mpambano wa kusisimua ajabu na hasa kwavile, Brazil ikitia bao, Ujerumani ikijibisha hadi Adriano alipotia bao la 3 lililoupiga msumari wa mwisho katika jeneza la Ujerumani katika Confederations Cup.Ujerumani chini ya kocha mpya Jürgen klinsmann hatahivyo, imepiha hatua mbele na kujenga timu mpya inayoegemea chipukizi na mastadi wa zamani akina Michael ballach na Oliver kahn.Wapya ni pamoja na Lukas Podolski wa FC Cologne na Schweinsteiger wa Bayern Munich.Ujerumani itarudi uwanjani kesho kwa changamoto na Mexico kuania nafasi ya tatu katika Kombe hili.

Katika changamoto za kombe la klabu bingwa barani Afrka:Ajax cape Town ya Afrika Kusini imewazima mabingwa wa afrika Enyimba wa Nigeria sare bao 1:1 hapo jana.Enyimba ilitishia kutamba mbele ya Ajax kwa kuitia shindo kubwa hatua za kwanza na ikatia bao mnamo dakika ya 9 ya mchezo.Ajax cape Town ikasawazisha mnamo dakika ya 17 ya mchezo.

Wanariadha wakiume wa Kenya walitia fora katika mbio za hapo jana za Km 10 mjini Jakarta,Indonesia wsakati wasichana wa Russia walitamba upande wa wanawake.Kenya ilinyakua nafasi zote 3 za usoni upande wa wanaume katika mbio zilizoandaliwa kuadhimisha mwaka wa 478 wa jiji la Djakarta.Ushindi ulikwenda kwa Wilberforce Talei,Mtei Enock na Stanley Kipkoger Salil.Talel alichukua muda wa dakika 28 na sek.48 kushinda.

Lydia Grigorieva wa russia alinyakua ushindi upande wa akina dada.Mshindi katika kila upande alijipatia kitita cha dala 11.000 huku mshindi wapili akipata dala 6000 na watatu 4000.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW