1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FINALI YA KOMBE LA KLABU BINGWA AFRIKA

27 Oktoba 2005

Duru ya kwanza ya finali ya ya Kombe la klabu bingwa barani Afrika kati ya Al Ahly ya Misri na Etoile Sahel ya Tunisia,itachezwa jumamosi hii mjini Sousse,Tunesia.

Katika Kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani,mabingwa Bayern Munich waliponea jana chupuchupu wasipigwe kumbo na mkenya bingwa wa mara 2 wa New York marathon, Margaret Okayo,amejitoa katika mbio zijazo za NY marathon.

Timu ya daraja ya pili ya Bundesliga-Hansa Rostock ilitoka nyuma jana na mwishoe ikaitimua

Stuttgart kwa mabao3:1 nje ya Kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani.Pigo hilo limemzushia balaa zaidi kocha mtaliana Giovanni Trapattoni.

Ilikua kwanza Stuttgart iliotangulia kutia bao kupitia Thomas Hitzlsperger,lakini Rostock ikajibisha kwa mabao 3 kabla kumalizika kipindi cha kwanza.

Sio tu Stuttgart bali hata MSV Duisburg imepigwa kumbo nje ya Kombe hili ilipozabwa mabao 3-2 na Munich 1860.

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich, nusra wakione kilichomtoa kanga manyoya mbele ya timu ya daraja ya pili ya Ligi Erzgebirge Aue.Mwishoe, Michael Ballack aliwaokoa kwa bao la kichwa mnamo dakika ya 80 ya mchezo.

Sasa Munich inaendelea kutamba katika vikombe 3-Bundesliga,Kombe la klabu bingwa barani Ulaya-champions League na Kombe hili la shirikisho.Hamburg ilitamba mbele ya Bayer Leverkusen na kuondoka na ushindi wa mabao 3-2 wakati Berlin iliitimua nje ya Kombe Borussia Mönchengladbach kwa mabao 3:0.

Eintracht Frankfurt ilizusha maajabu mengine ilipoicharaza Schalke 04-makamo-bingwa wa Ujerumani mabao 6:0.Ni wiki 1 tu kabla pale Frankfurt ilipoizaba FC Cologne pia mabao 6:3.

Kocha wa Taifa wa ujerumani,Jürgen Klinsmann amearifu yutayari kubakia zaidi kocha wa Ujerumani baada ya kombe lijalo la dunia iwapo Ujerumani itacheza uzuri katika Kombe hilo.

Ni mara ya kwanza kwa Klinsmann aliechukua mahala pa Rudi Völler,kutoa ishara ya kutaka kubakia zaidi kocha wa Ujerumani.Palikuwapo mvutano kati ya Klinsmann na mameneja wa klabu za Bundesliga na hivyo walikutana majuzi kutatua mataizo yao.

Keshokutwa jumamosi asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo-mkutano mjini Sousse,Tunisia.Al Ahly ya Misri itajaribu kushinda mpambano wake wa 50 mfululizo na kuseleleza rekodi yake ya kutoshindwa kipindi cha miezi 15.Itakuwa uwanjani katika duru ya kwanza ya finali ya Kombe la klabu bingwa kati yake na Etoile Sahel.Huu utakua mtihani mgumu kwa mabingwa hao wa Misri.Etoile lakini inacheza nyumbani na inataka kuiigiza timu ya taifa ya Tunesia kuliwakilisha bara la Afrika katika Kombe la dunia la klabu bingwa hapo desemba mjini Tokyo,Japan.

RIADHA:

Bingwa mara mbili wa New york marathon kutoka Kenya, Margaret Okayo amejitoa katika mbio za mwaka huu za NY marathon zitakazofanyika Nov.6.Ameumia.

Amesema kwamba, hakupona sawa sawa kuweza kuhimili vishindo vya mbio hizo.Okayo alikuwa mmoja wa wale waliotazamiwa kushinda mara hii tena.Alishinda New York marathon 2001 na tena 2003 na ndie mwenye rekodi ya mbio hizo upande wa wanawake ya muda wa masaa 2:22:31.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW