1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FINALI YA KOMBE LA KLABU BINGWA:ETOIL SAHEL YAICHAPA MABINGWA ENYIMBA 2-1.SCHALKE KILELENI MWA BUNDESLIGA NA MASHINDANO YA DUNIA YA RIADHA BERLIN 2009.

Ramadhan Ali6 Desemba 2004

MICHEZO MWISHONI MWA WIKI:

Katika Bundesliga-Ligi ya Ujerumani,Schalke 04 ikiwa na washambulizi 2 hatari Gerald Assamoha wa asili ya Ghana na Mbrazil Ailton,iliikomea jana Borussia Dortmund,mabingwa wa 1997 na 2001 bao 1-0 na kuparamia kileleni mwa Ligi wakiwa sawa kwa pointi na Bayern Munich.Bao la Ailton la dakika ya 17 ya mchezo, lilitosha kuwatumbuiza mashabiki 83,000 katika uwanja wa Westfalenstadion mjini Dortmund.

Bayern Munich ilimudu suluhu tu mabao 2:2 na Nüremberg hapo jumamosi.katika mpambano mwengine wa hapo jana wa Bundesliga,Kaiserslauten iliichapa Mainz mabao 2 na hivyo imejikomboa kutoka mkiani mwa Ligi na hatari ya kuteremshwa daraja ya pili.

Ama katika Ligi ya Uingereza,Chelsea inaendelea kushika usukani kuweza kuvaa taji lao la kwanza la Premier League tangu kupita miaka 50.Chelsea iliibomoa Newcastle kwa mabao 4-0 hapo jumamosi na sasa iko pointi 5 mbele ya mabingwa Arsenal.

  • Huko Ufaransa,Olympique Marseille,ilinyakua ushindi wake wa kwanza chini ya kocha wao mpya Phillipe Trousier ilipoizaba Caen mabao 3-2.Mabingwa na viongozi wa Ligi Olympique L yon wameendeleza rekodi yao ya kutofungwa msimu huu hadi mechi 17,ingawa walimudu suluhu tu bao 1-1 na AC Ajaccio.

Ama katika Serie A,Ligi ya Itali, Juventus inaendelea kuongioza kwa pointi 4 kileleni,lakini walipaswa kutoka nyuma ili kuizima Lazio Roma hapo jana kabla kutia mabao 2-1.

Na katika La Liga au Ligi ya Spain,FC Barcelona shukurani kwa mabao 2 ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika,mkamerun samuel Eto’o.Barcelona iliizaba Malaga mabao 4:0.

na nchini Hololand,PSV Eindhoven ilikumta timu ya mkiani mwa ligi Graafschap Doetinchem mabao 4-0.

Kesho ni zamu ya duru nyengine ya Champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya:Klabu 3 maarufu za Ulaya huenda zikafunga virago na mapema:Arsenal London,Liverpool na Real Madrid. Mabingwa wa Uingereza Arsenal,wakiwa nafasi ya pili katika kundi E wanakutana na timu ya mkiani Rosenborg ya Norway wakijua lazima washinde au la kwaheri.Keshokutwa jumatano,Liverpool inaelewa pia lazima ishinde mbele ya Olympiakos ya Ugiriki,viongozi wa kundi lao.Real Madrid nayo,mabingwa mara 9 wa Ulaya,wanakutana na Roma ya Itali na ushindi utawasukuma usoni,lakini wakimudu sare tu huko Itali,basi bayer Leverkusen ya Ujerumani itajiunga na Dynamo Kiev duru ijayo wakitoka suluhu na waukaraini.

KOMBE LA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA:

Duru ya kwanza ya finali ya Kombe la klabu bingwa barani afrika imemalizika kwa ushindi wa kutatanisha wa mabao 2-1 wa Etoile du sahel ya Tunisia mjini Sousse dhidi ya mabingwa Enyimba wa Nigeria.Timu zote 2 kwa ,kweli zilitoka uwanjani zikiwa na wachezaji 10 kila upande.Etoile walitoka nyuma walipozabwa bao na Enyimba n a mwishoe kuwatimua wanigeria ambao walikuwa wakwanza kupoteza mnchezaji 1 tayari mnamo dakika ya 31 ya mchezo.

Finali hii ilijionea maamuzi kadhaa ya kutatanisha ya rifu kutoka Algeria Mohamed Benouza.Enyimba iliongoza kutia bao pale Nwanna alipolifum,ania lango la Sahel.Lakini,ikawa kutangulia si kufika, kwani bahati ya mabingwa Enyimba iliingia dosari kwa kutolewa nje ya uwanja na rifu kwa kwa stadi wao Okonkwo mnamo dakika ya 31 ya mchezo.Etoile wa kutunukiwa mkwaju wa bure wa penalty na wa kutatanisha mara tu baada ya kipindi cha mapumziko.Halafu dakika 8 baada ya mapumziko Etoile du sahel ikatia bao la pili na kuiarifu Enyimba imejiwinda kuivua taji.

Lakini Eynimba inadai pia kutangulia si kufika,ni duru ya pili wiki ijayo mjini Abuja,itakayoamua hatima ya Kombe hili mwaka huu.Kwani, Enyimba inapigania kuwa klabu ya kwanza ya Afrika kulin ‚gan’gania Kombe tangu pale Englbert ya Zaire kuthubutu kufanya hivyo 1967 na 1968.

Mjini Yaounde, Cameroun,Conton Sport ndio mabingwa wapya msituni mwa simba wa nyika:Kwa mara ya pili mfululizo,canton Sport wamenguruma jana mbele ya mahasuimu wao Tonnerre Yaounde.Aloma alipiga hodi mara 3 na kuitikiwa katika ushindi huo wa mabao 4-1.

WACHEZAJI 2 WAFARIKI DUNIA:

Mmorocco Hicham Zerouali,aliewahi kuichezea klabu ya Aberdeen ya scvotland,alifariki jana dunia katika jali ya motokaa mjini Rabat aliposhindwa kuudhibiti usukani wa gari yake na kujigonga na mit.

Mchezaji huyo wa Taifa wa Morocco alikua na umri wa miaka 27 na siku 1 kabla alitia mabao 2 pale klabu yake Royal Armed Forces iliposhinda mpambano wa Ligi.

Na taarifa kutoka New Delhi,India, zasema mzaliwa wa Brazil-Cristiano Junior,aliekua na umri wa miaka 24 tu,alipinduka ghafula na kufariki dakika tu baada ya kutia bao lake la pili kwa klabu yake Dempo ya Bangalore .Cristiano aonesha aligongana na kipa Mohun Bagan wakati akitia bao lake hilola pili na la ushindi.

MASHINDANO YA RIADHA YA UBINGWA WA DUNIA 2009 YATAFANYIKA BERLIN:

Mji wa Berlin, ukisherehekea jana ushindi wa kuandaa mashindano ya ubingwa wa riadha ulimwenguni-world athletics championship 2009.

Siku 2 tu kabla, kocha wa timu ya Taifa ya dimba ya Ujerumani, Jürgen Klinsmann alitangaza mji wa Berlin utakua ndio kambi ya timu yake ya Taifa kujiandaa kwa Kombe la dunia 2006 litakalochezwa pia Ujerumani.

Mji wa Berlin umeishinda miji ya Valencia na Split.Uwanja wa Berlin umeshajengwa tayari kwa mashindano hayo na hapo Septemba ukiwa na safu ya kukimbilia ya rangi ya buluu ,uwanja wa Olimpik wa Berlin, ulikuwa kilele cha mashindano ya Golden League,kilele cha msimu wa riadha.Mji wa Berlin ulichaguliwa kwa kura 24 kati ya zote 26 zilizopigwa.

Mashindano kama haya ya ubingwa wa riadha duniani-Gebre Selassie.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW