SiasaFinland
Finland ina matumaini ya kujiunga na NATO
30 Januari 2023Matangazo
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Finland Pekka Haavisto amewaambia wandishi habari mjini Helsinki kuwa dhamira ya serikali ya nchi hiyo ni kuona Finland na Sweden zinajiunga pamoja ndani ya NATOna msimamo huo haujabadilika.
Serikali ya Uturuki ambayo bado inajivutavuta kuridhia azimio la kuzikaribisha nchi hizo mbili ndani ya NATO, ilishupaza msimamo wake kuhusu Sweden baada ya kisa cha wiki iliyopita ambapo mwanasiasa wa mrengo mkali nchini Swedenaliichoma moto Quran Tukufu mbele ya ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm.
soma pia:Erdogan ameashiria ataunga mkono kuikaribisha Finland NATO
Kufuatia kitendo hicho rais Erdogan alisema Sweden haiwezi tena kuitegemea Uturuki kuisaidia kupata unachama wa NATO.