JamiiFinland
Finland nchi yenye furaha zaidi duniani
20 Machi 2023Matangazo
Kulingana na Ripoti ya Furaha Duniani iliyochapishwa leo, Finland inafuatiwa na Denmark, Iceland, Israel, Uholanzi, Sweden, Norway, Uswisi, Luxembourg na New Zealand.
Ripoti hiyo ambayo imeangazia athari za mzozo wa virusi vya corona kwa ustawi wa watu, huandaliwa kila mwaka na wanasayansi wa Marekani kwa kuzingatia utafiti unaofanywa na Taasisi ya Gallup.
Austria na Australia zimeshika nafasi ya 11 na 12, huku Ujerumani ikishika nafasi ya 16, ikishuka kwa nafasi mbili katika ripoti ya mwaka jana. Utafiti huo umeeleza kuwa Afghanistan na Lebanon zimeendelea kuwa nchi mbili zisizo na furaha.