FISHER MASHARIKI YA KATI
16 Desemba 2003Matangazo
BERLIN: Waziri wa nje wa Ujerumani Joscha Fischer,ameanza ziara ya siku 3 katika Mashariki ya Kati.Huko anatazamiwa kukutana na viongozi wa Misri,Jordan,Israel na wa Mamlaka ya Ndani ya wapalestina. Katika hatua yake ya kwanza ya ziara yake, Fischer anatazamiwa kuwa na mazungumzo na rais Hosni Mubarak wa Misri na baadae hii leo anatarajiwa kuwasili Jordan.
