1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fisi wauwa, wajeruhi Kenya

7 Februari 2024

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na kundi la fisi karibu na chuo kimoja kikuu nje kidogo ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Fisi wauawa na kujeruhi nchini Kenya.
Fisi wauawa na kujeruhi nchini Kenya.Picha: C. Piek/blickwinkel/AGAMI/picture alliance

Mmoja wa waliojeruhiwa ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Multimedia aliyeshambuliwa katika barabara moja inayopakana na Mbuga ya Kitaifa ya Wanyama ya Nairobi huko Ongata Rongai.

Kisa hicho kimepelekea wanafunzi kutoka chuo hicho kuandamana wakilalamikia usalama wao. Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wananfunzi hao.

Shirika la Wanyama Pori nchini Kenya (KWS) linasema kikosi kilichotumwa kuchunguza kisa hicho kilipata sehemu za mwili wa mtu katika eneo la tukio.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW