Watano wafariki katika mashambulizi ya Urusi na Ukraine
9 Agosti 2026
Matangazo
Vita vya Urusi dhidi ya Ukraine vimeendelea kuchukua sura mpya wakati mashambulizi kutoka pande zote mbili yakiendelea kuvurumishwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hizo.
Usiku wa kuamkia leo nchini Ukraine shambulio la Urusi limewaua watu wawili na kuwajeruhi wengine 23 katika mji wa kaskazini wa Kharkiv, hayo yamesemwa na gavana wa mji huo Oleg Synegoubov.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema katika mtandao wa kijamii wa X kwamba washirika wa nchi yake ni lazima sasa waipatie nchi yake msaada wa mifumo ya ulinzi wa anga na kuiwekee vikwazo zaidi Urusi.
Urusi nayo kwa upande wake imeripoti vifo vya watu watatu na majeruhi 25 katika mji wa mpakani wa Belgorod kufuatia shambulio la droni la Ukraine.