1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FRANKFURT AM MAIN: Wasaidizi wa kwanza wa kijerumani wameondoka

27 Desemba 2003
kuelekea eneo lililoathirika kwa mtetemeko wa ardhi nchini Iran. Kwa mujibu wa msemaji wa shirika la ushirikiano wa kiufundi, ndege iliondoka jana jioni mjini Frankfurt, ikiwa na makundi ya waokozi, wataalam wa tiba wa chama cha msalaba mwekundu, na shirika la utoaji misaada MALTESER sawa na majibwa ya kusaidia kazi za uokozi. Isistoshe ndege ina shehena za nguo na mablanketi ikielekeo eneo hilo la msiba. Kadhalika nchi kadhaa wa kadhaa, ikiwamo Marekani, zimeahidi misaada. Muungano wa Ulaya unachangia msaada wa dharura wa EURO laki nane.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW