FRANKFURT : Madereva wa treni kugoma
6 Agosti 2007Matangazo
Madereva wa treni nchini Ujerumani wamepiga kura leo hii kwa kauli moja kufanya mgomo kuhusiana na suala la mishahara ambao unatishia kutibuwa kabisa usafiri wa mamilioni ya abiria katika kilele cha msimu wa mapumziko.
Migomo hiyo itakuwa mikubwa kabisa kuwahi kulikumba shirika la reli la Ujerumani Deutsche Bahn katika kipindi cha miaka 15 kwanza itaathiri usafiri wa mizigo na pengine baadae usafiri wa abiria.
Manfred Schell mkuu wa chama cha wafanyakazi cha madereva wa treni amesema wanachama wake wameshindwa kufikia makubaliano ya mishahara na shirika la Deutsche Bahn na kwamba asilimia 95 nukta nane ya wanachama hao wameunga mkono mgomo huo.
Amesema wanalipa shirika hilo la reli hadi Jumanne kuboresha madai yao na kuepusha mgomo huo.