Frankfurt. Mgomo wa madereva wa treni waendelea.
15 Novemba 2007Mgomo wa madereva wa treni nchini Ujerumani kwa treni za mizogo , ambao unafanyika tangu mchana jana , umeilazimisha kampuni ya magari ya Audi kufuta shift yake ya kazi katika kiwanda chake mjini Brussels leo Alhamis. Kampuni hiyo imesema kuwa wafanyakazi 800 wametakiwa kubakia nyumbani kwasababu treni mbili zikiwa na vifaa vya magari kutoka Slovakia yamekwama upande wa mashariki ya Ujerumani. Wakati huo huo , umoja wa madereva wa treni GDL umesema mgomo wa madereva wa treni za abiria na treni za masafa ya mbali utaanza mapema leo. Umoja huo unadai asilimia 30 ya nyongeza ya mshahara na umekataa kurejea katika meza ya majadiliano hadi pale uongozi utakapoongeza pendekezo lake la asilimia 10 la nyongeza ya mshahara ili kuweza kukubaliana juu ya ongezeko la saa za kazi kwa wiki.