Frankfurt. Mgomo waendelea.
16 Novemba 2007Matangazo
Abiria nchini Ujerumani wamekuwa wakipata usumbufu kutokana na mgomo wa hivi sasa wa madereva wa treni ulioitishwa na umoja wa wafanyakazi hao wa GDL unaokusudia kutia mbinyo zaidi kwa madai yao ya ongezeko la asilimia 30 ya mshahara . Mgomo huo unaathiri abiria pamoja na mazigo, na utaendelea hadi mapema kesho Jumamosi.
Shirika la reli nchini Ujerumani , Deutsche Bahn linaendesha huduma ya dharura hadi wakati huo. Mgomo kwa ajili ya treni za mizigo umeshaanza kuathiri uchumi. Kiwanda cha utengenezaji wa magari ya Audi nchini Ubelgiji tayari kimesitisha shifti kadha za kazi kwasababu sehemu muhimu za magari hazijawasili.