FRANKFURT : Mwandishi wa Israel atunukiwa Tuzo ya Goethe
28 Agosti 2005Matangazo
Mji wa Frankfurt nchini Ujerumani umemtunuku Tuzo ya Hadhi ya Goethe kwa mwaka 2005 mwandishi wa Israel Amos Oz kwa utambuzi wa mafanikio aliyopata katika maisha yake akiwa kama mwandishi.
Oz alipokea tuzo hiyo ambayo inaadamana na fedha taslimu euro 50,000 kwenye kanisa la St.Paul lilioko katika mji mkuu huo wa kibiashara wa Ujerumani.Tuzo hiyo hutolewa kila baada ya miaka mitatu na inahesabiwa kuwa mojawapo ya tuzo za juu za fasihi barani Ulaya.
Kazi za mwandishi huyo wa Israel mwenye umri wa miaka 66 ni pamoja na riwaya Black Box na To know a woman ambavyo vimetafsiriwa kwa lugha 30.Oz ni mtetezi mkubwa wa suluhisho la amani kwa mgogoro kati ya Israel na Wapalestina.