FRANKFURT:Kansela Merkel asisitiza kutunza mazingira
14 Septemba 2007Matangazo
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amewaahidi watengeneza magari wa Ujerumani kuwa atawaunga mkono katika mvutano kati yao na halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya kuhusu maswala ya kuhifadhi hali ya hewa, wakati huo huo kansela Merkel akifungua maonyesho ya kimataifa ya magari mjini Frankfurt amewataka watengeneza magari wa Ujerumani wachunguze vipi moshi wa viwandani unaochafua mazingira na jinsi utakavyoweza kupunguzwa.
Kansela Merkel amesisitiza kuwa ni lazima tukabiliane na mabadiliko ya hali ya hewa.