1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
KandandaUjerumani

Freiburg yawashinikiza Bayern na Dortmund

9 Novemba 2026

Freiburg wamezidi kuwawekea shinikizo vinara wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga Bayern Munich na Borussia Dortmund.

Kandanda-Bundesliga 2026/27 | SC Freiburg vs. Union Berlin | mapambano na Yuito Suzuki
Yutio Suzuki wa Freiburg (kulia) akipambana na wachezaji wa Union BerlinPicha: Philipp von Ditfurth/dpa/picture alliance

 Hii ni baada ya kupata ushindi wa 2-0dhidi ya Union Berlin na kurudi kwenye nafasi ya tatu katika msimamo.

Nahodha wa Union Rani Khedira aliwekewa shinikizo na Freiburg na akaishia kufunga katika lango lake kunako dakika ya tisa ya mechi na baada ya muda wa mapumziko Yuito Suzuki akapachika bao la pili na kuwapalekea kupata ushindi licha ya nahodha wao Vincenzo Grifo kukosa mkwaju wa penalti.

Dabi ya Mto Rhine yachezwa mjini Köln

Freiburg ambao walifungwa kwenye fainali ya Ligi ya Ulaya na Aston Villa msimu uliopita kwa sasa wanaishikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na pointi 19, pointi mbili nyuma ya Bayern na Borussia Dortmund, huku miamba hao wa Bavaria wakiwa kileleni kutokana na wingi wa mabao.

Yutio Suzuki akisherehekea kuifungia Freiburg baoPicha: Fernando Gutierrez-Juarez/dpa/picture alliance

"Tulijua nafasi zetu zitakuja na tulifanikiwa kuzitumia," alisema Derry Scherhant winga wa Freiburg.

Mapema Jumapili, Bayer Leverkusen waliwazidi nguvu FC Köln katika dabi ya Rhine kwa kupata ushindi wa 2-1 mjini Köln, ambao uko kilomita 10 tu kutoka Leverkusen.

Leverkusen walifungiwa mabao yao na Aleix Garcia na Patrik Schick kisha Köln wakafungiwa na Said El Mala katika dakika ya mwisho ya mechi.

Mechi hiyo yenye uhasama mkubwa ilishuhudia wachezaji 11 kuonyeshwa kadi za njano, sita kati ya kadi hizo zikiwaendea wachezaji wa nyumbani FC Köln.

Köln yazidi kushuka kwenye jedwali

Kushindwa huko kwa Köln kunaishusha timu hiyo hadi katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wakiwa na pointi 9 huku Leverkusen wakitua katika nafasi ya tano kwenye msimamo pointi zao zikiwa 16.

Mchezaji wa FC Köln Said El Mala akiwa amezingirwa na wachezaji wa LeverkusenPicha: Rolf Vennenbernd/dpa/picture alliance

Katika mechi ya mwisho ya Jumapili TSG Hoffenheim waliwalaza Schalke 04 2-1 huku Fisnik Asllani na Tim Lemperle wakifunga mabao ya hao wenyeweji.

Imehaririwa na:Babu Abdalla
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW