Frof. Zibakalam atunukiwa tuzo ya Uhuru wa habari
3 Mei 2018Profesa Zibakalam hii sio mara ya kwanza kuingia matatani na serikali . Na kutokana na ujasiri wake wa kuikosoa serikali ya Iran Zibakalam ametunukiwa tuzo ya uhuru wa kutoa maoni uhuru wa vyombo vya habari.
"Nafikiri kosa langu ni kwamba katika mahojiano na DW nilizungumzia kuhusu masuala ya kisiasa, mawazo ambayo serikali inayapinga", amesema Sadegh Zibakalam. Wakati serikali ikisema, kwamba machafuko nchini Iran yanatokana na maadui wa nchi hiyo, serikali inatarajia, kwamba kila mmoja atafuata msimamo huo na kuurudia."
Sadegh zibakalam hajafanya hivyo. Mwezi Januari alisema mtaalamu huyo wa masuala ya siasa kutoka Iran katika mahojiano na DW idhaa ya Kifarsi kuhusiana na hali ya machafuko wakati ule nchini Iran.
Wakati huo Wairan zaidi ya 10,000 waliingia mtaani , wakipinga sera za kiuchumi pamoja na uongozi mzima wa kisiasa nchini humo. Zibakalam alionesha kuwaelewa waandamanaji pamoja na kupinga shutuma za serikali. "Nasema , kwamba maandamano yalipangwa na kuongozwa na Wairan wenyewe. Na hakuna kabisa mtu yeyote kutoka nje ya Iran aliingiza ushawishi wake. Kwa kweli hakuna ushawishi wa nje katika maandamano hayo", alisema Zibakalam katika mahojiano na DW. Kutokana na hayo Zibakalam mwenye umri wa miaka 69 anakabiliwa na kifungo cha miaka 18.
Zibakalam kutengwa kijamii
Mwezi Machi mahakama ya serikali ya mapinduzi ya Iran ilitoa hukumu hiyo dhidi ya Zibakalam. Iwapo itathibitishwa, mtaalamu huyo wa kisiasa hatafungwa tu jela, lakini pia atakabiliwa na adhabu ya miaka miwili ya kutengwa kijamii. Hii ina maana , Zibakalam hataweza kufanya mahojiano na chombo chochote cha habari , na hataweza kuandika makala yoyote kwa umma.
Na pia hataruhusiwa kutumia mitandao ya kijamii kwa muda wa miaka miwili. Zibakalam amekata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, hata hivyo uamuzi bado haujachukuliwa. Hadi wakati huo atakaa kimya, kujilinda? Kwa Zibakalam inaonekana kwamba hilo sio njia anayoitaka. Adhabu hiyo inayomkabili hamshughulishi mtaalamu huyo wa masuala ya siasa, na kila siku yuko katika ukurasa wa Twitter na Facebook na kutoa maneno ya ukosoaji wa wazi.
"Wakati mahakama itakaponiambia : Profesa Zibakalam, huruhusiwi kufanya mahojiano tena, hapo ndio nitaacha. Lakini hilo hawajalifanya. Ndio sababu nasubiri hadi sasa, hadi pale mahakama ya rufaa itakapotoa uamuzi wao," amesema hayo katika mahojiano na DW.
Mhalifu sugu
Kwa upande wa mahakama nchini Iran Zibakalam ni mhalifu anayerejea uhalifu kila mara. Profesa huyo wa chuo kikuu cha mjini Tehran ni mmoja kati ya wasomi maarufu na wataalamu wa siasa nchini Iran. Zibakalam ni mmoja kati ya watu waliomo katika kundi la wanamageuzi walioko karibu na rais Hassan Rouhani.
Anafahamika kwa jinsi anavyoweza kuendesha majadiliano akiwa na msimamo mkali. Na pia amekuwa akiikosoa serikali katika sera zake za siasa za nje na pia misimamo ya serikali. Mwezi Februari 2014 aliwahi kusema, kuhusu kuitambua Israel kama taifa na pia Marekani. Zibakalam amekuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha masuala ya kisiasa nchini Uingereza cha Brandford. Katika maandishi yake aliandika kuhusu "mapinduzi ya Kiislamu na siasa za mataifa ya magharibi".
Wakati akiwa mwanafunzi mwaka 1974 alitembelea nchini mwake na kukamatwa na askari kanzu wa Shah, kutokana na kuihujumu nchi pamoja na kutoa propaganda. Baada ya mapinduzi ya Kiislamu alirejea nyumbani mwanzoni mwa miaka ya 1980. Miaka michache baadaye alianza kazi yake katika chuo kikuu cha Iran mjini Tehran. Mwaka 2000 aligombea katika uchaguzi wa bunge nchini Iran katika mji wa Zanjan kaskazini magharibi mwa Iran. Hata hivyo hakuruhusiwa kugombea na baraza la kuchuja wagombea la taifa.
Mwandishi: Rahel klein / ZR / Sekione Kitojo
Mahriri: Mohammed Abdul-Rahman