1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mario Gotze: Nilifanya makosa kurejea Dortmund

21 Septemba 2023

Mshindi wa Kombe la Dunia la mwaka 2014, Mario Götze, ameweka wazi kwamba kurejea kwake Borussia Dortmund mwaka wa 2016 yalikuwa ni makosa anayoyajutia na kwamba ni bora angetafuta timu nyingine nje ya Ujerumani

Fußball Bundesliga VfB Stuttgart gegen Borussia Dortmund Flash-Galerie
Mario Goetze alipokuwa akikipiga Borussia DortmundPicha: dapd

Götze anakiri kurudi Dortmund mnamo 2016 ilikuwa makosa.

Mshindi wa Kombe la Dunia la mwaka 2014, Mario Götze, ameweka wazi kwamba kurejea kwake Borussia Dortmund mwaka wa 2016 kwamba yalikuwa ni makosa anayoyajutia.

"Labda ni uamuzi wa kurudi nyuma kwenda Dortmund. Nilipaswa kufanya uamuzi tofauti'', alisema alipoulizwa na podkasti ya Spielmacher kuhusu kosa alilofanya katika fani yake.

Soma zaidi:  Götze kujiunga na Eintracht Frankfurt

"Nilikuwa na chaguo moja au mawili, pia Liverpool kujiunga na Jürgen hatua ya nje ya Ujerumani, baada ya kucheza huko Dortmund na Bayern ingekuwa nzuri. Hivyo ndivyo nilifanya miaka minne baadaye, kupata tu ushindani mpya.'' Aliongeza.

Mario Goetze anakukumbukwa kwa goli lake lilioipa ubingwa wa dunia timu ya taifa ya Ujerumani mwaka 2014 huko Rio De Jeneiro Brazil.Picha: dapd

Mario Götze, ambaye sasa yuko katika timu ya Eintracht Frankfurt, alisababisha ghadhabu na sintofahamu alipohama Borussia Dortmund kwenda kwa wapinzani wao Bayern Munich mwezi mmoja kabla ya mechi Fainali ya Ligi ya Mabingwa 2013 kati ya timu zote mbili.

Soma zaidi:Bayern Munich yakosolewa dili lake la Visit Rwanda 

Baada ya miaka mitatu na Bayern Munich, alirudi tena Dortmund lakini hakuwa tena na hali nzuri na timu hiyo na baada ya muda mfupi alihamia PSV ya Uholanzi kabla ya kurejea tena Bundesliga kujiunga na Frankfurt mnamo 2022.

Götze, ambaye alifunga bao la ushindi la Kombe la Dunia la 2014 kwa Ujerumani, alisema
"ingekuwa vizuri" kucheza nje ya nchi wakati huo, akiongeza kwamba alipata shinikizo kubwa kutoka vyombo vya habari baada ya kufunga goli hilo la kukumbukwa mjini Rio de Janeiro, Brazil.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW