1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

G20 inakubali uanachama wa Umoja wa Afrika

7 Septemba 2023

Mataifa 20 yaliyostawi na yanayoinukia kiuchumi G20, yamekubaliana kuipa uanachama wa kudumu Umoja wa Afrika.

Indien | G20-Gipfel in Neu-Delhi
Picha: Amarjeet Kumar Singh/AA/picture alliance

Kwa mujibu wa shirika la habari la Bloomberg likivinukuu vyanzo vyenye ufahamu na suala hilo imesema, hatua hiyo itaupa umoja wa Afrika hadhi sawa na Umoja wa Ulaya.

Soma pia: Waziri mkuu wa India atoa mwito wa Umoja wa Afrika kujiunga kwenye kundi la G20

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi aliwaandikia viongozi waG20 mwezi Juni akipendekeza Umoja wa Afrika kujumuishwa katika kambi hiyo wakati wa mkutano wa kilele utakafanyika New Delhi, India mwishoni mwa juma.

Kwa sasa Kundi hilo linajumuisha nchi wanachama 19 na Umoja wa Ulaya.

Kundi la G20 mwaka huu pia limeyaalika mataifa 9 yasiyo wanachama yakiwemo Bangladesh, Singapore, Uhispania na Nigeria, na mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Shirika la Afya Duniani, Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW