1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

G20 yarefusha muda wa mataifa maskini kulipa madeni

15 Oktoba 2020

Mataifa tajiri duniani ya kundi la G20 yamekubaliana kurefusha kwa miezi sita muda wa kusitisha ulipaji madeni kwa mataifa maskini yaliyoathiriwa na janga la virusi vya corona.

Japan Osaka G20 Gipfel Joko Widodo Präsident Indonesien
Picha: President Secretary/Laily Rachev

Hiyo ni tofauti na miito iliyotolewa na Benki ya Dunia na watetezi wengine ya kutaka muda huo urefushwe kwa mwaka mmoja. Wakati wa mkutano uliofanyika kwa njia ya video, mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu kutoka mataifa ya kundi la G20 wameridhia kusogeza mbele hadi Juni 2021 muda wa mwisho kwa mataifa masikini kuanza tena kulipa madeni yake ili kuzisaidia nchi hizo kupambana na janga la COVID-19.

Waziri wa fedha wa Saudi Arabia Mohammed al-Jadaan aliyekuwa mwenyeji wa mkutano wa G20 amesema ingawa uchumi wa dunia unaimarika taratibu, mataifa masikini bado yanakabiliwa na hali mbaya kutokana na athari za janga la COVID-19. Usimamishaji wa kulipa madeni ulikuwa unafikia tamati Novemba mwaka huu na kundi la G20 limesema muda wa nyongeza uliokubaliwa jana unaweza kurefushwa tena wakati wa majadiliano yatakayofanyika wakati wa majira ya kiangazi mwaka 2021.

Benki ya dunia ilisema mwanzoni mwa wiki hii kwamba madeni katika nchi 73 maskini yaliongezeka kwa asilimia 9.5 mwaka jana hadi kufikia dola bilioni 744.

   

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW