1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiBrazil

G20 yaweka mikakati kuwatoza kodi matajiri wakubwa duniani

27 Julai 2024

Mawaziri wa fedha kutoka nchi zilizoendelea kiviwanda duniani G20 wamekubaliana kwa kauli moja kuweka mikakati ya kuwatoza ushuru matajiri wakubwa duniani.

Canada | Melanie Joly
Waziri wa fedha wa Canada Melanie Joly akihudhuria mkutano wa G20 mjini Rio de Janeiro, Brazil.Picha: Silvia Izquierdo/AP/picture alliance

Katika taarifa yao, mawaziri hao wamesema wanasaka uwiano wa kimataifa na ushirikiano zaidi juu ya kuziba mianya ya matajiri wakubwa kukwepa kulipa kodi.

Brazil inayoshikilia urais wa kupokezana wa kundi la G20, ilitoa pendekezo la kuwatoza ushuru wa asilimia mbili watu wenye utajiri unaozidi dola bilioni moja za Kimarekani.

Soma pia: Oxfam: Matajiri duniani waongeza utajiri wao

Licha ya kutokubaliana kuhusu kiwango maalum cha ushuru, waziri wa fedha wa Brazil Fernando Haddad amesema wamepiga hatua muhimu.

Pendekezo la kuwatoza ushuru watu wenye utajiri uliopindukia limeibua mgawanyiko miongoni mwa nchi wanachama wa G20.

Ufaransa, Uhispania na Afrika Kusini zimeunga mkono japo Marekani imepinga pendekezo hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW