SiasaJapan
G7 inapanga juhudi mpya za chanjo kwenye nchi zinazoendelea
13 Mei 2023Matangazo
Gazeti la Japan, Yomiuri limeripoti Jumamosi kuwa mpango huo mpya unakusudia kukusanya fedha kwa ajili ya kutengeneza na kununua chanjo, pamoja na kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya, ili kujiandaa kwa janga lijalo la kimataifa.
Katika mkutano wa Jumamosi wa mawaziri wa fedha na mawaziri wa afya wa G7, wamekubaliana kutoa msaada kwa nchi zenye kipato cha chini na cha kati ili kusaidia kuongeza jukumu lao katika mfumo wa kusambaza bidhaa zinazohusiana na nishati.
Viongozi wa G7 watazingatia iwapo watoe tamko kuhusu jinsi ya kukabiliana na janga la kimataifa katika mkutano huo utakaofanyika kuanzia Mei 19 hadi 21, Hiroshima, Japan.