SiasaUkraine
G7 kutangaza mpango wa muda mrefu wa usalama kwa Ukraine
12 Julai 2023Matangazo
Tangazo hilo litatolewa pembezoni mwa mkutano wa NATO unaofanyika nchini Lithuania baada ya mazungumzo kati ya viongozi wa kundi la G7 na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine.
Duru zinasema kundi la G7 litaweka mezani mpango mpana wa kuipatia Ukraine silaha za kisasa za kivita, mafunzo kwa wanajeshi wake na kubadilishana taarifa za kiintelinjesia pamoja na ulinzi wa mifumo ya mawasiliano ya mtandao.
Kundi hilo linalojumuisha mataifa ya Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Japan, Canada na Italia linalenga kutumia mpango huo kutuma ujumbe mzito kwa utawala wa Urusi kwamba kamwe hawataitupa mkono serikali mjini Kyiv.