1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

G7 zaonya kuhusu athari za kubadilika thamani ya sarafu

8 Februari 2004
BOCA RATON: Mawaziri wa Mambo ya Fedha na Wakuu wa Benki wa nchi saba za viwanda katika kundi la G7 wameonya kuhusu athari za kubadilika badilika thamani za sarafu. Katika mkutano huo unaofanyika mjini Boca Raton mkoani Florida, Marekani ilipinga kuchukuliwa hatua yoyote ya kurekibishwa udhaifu wa hivi sasa wa thamani ya Dollar. Mitindo ya kusawazishwa thamani za sarafu katika masoko ya kimataifa ya fedha si muwafaka kwa ustawi wa uchumi, lilisema toleo la mwisho la mapatano hayo magumu. Kurekibishwa thamani za sarafu lazima kwende sambamba na marekibisho ya ustawi wa uchumi, liliendelea kusema toleo hilo. Barani Ulaya ulizidi wasi wasi kuwa sarafu ya EURO inazidi kupanda thamani kulinganishwa na Dollar ya Kimarekani. Upande wa pili nchini Marekani udhaifu huo wa Dollar hautazamwi kama tatizo mnamo mwaka huu wa uchaguzi wa Rais kwa sababu utachangia kuunyanyua ustawi huo wa uchumi wenye nguvu kabisa duniani.