1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gabon kufanya uchaguzi wa rais mwezi Aprili

23 Januari 2025

Serikali ya mpito nchini Gabon imesema itafanya uchaguzi wa rais Aprili 12, hii ikiwa ni hatua muhimu ya kuurejesha upya utawala wa kiraia baada ya mapinduzi yaliyohitimisha udhibiti wa miongo kadhaa wa familia ya Bongo.

Abstimmung über Verfassungsänderung in Gabun
Waangalizi wa uchaguzi nchini GabonPicha: NAO MUKADI/AFP

Msemaji wa serikali ya Gabon Serapin Akure Davain ametoa tangazo hilo mapema hii leo baada ya mkutano wa baraza la mawaziri.

Soma pia: Raia wa Gabon wapiga kura ya maoni kuhusu katiba mpya

Taifa hilo la Afrika lenye utajiri wa mafuta ambalo limetawaliwa na familia ya Bongo kwa miaka 55, ilipitisha katiba mpya katika kura ya maoni ya mwezi Novemba.

Rais wa mpito Jenerali Brice Oligui Nguema, aliyechukua wadhifa huo mara baada ya mapinduzi ya Agosti 2023, ameweka wazi azma yake ya kusalia madarakani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW