Gabon yapigia kura katiba mpya baada ya mapinduzi
16 Novemba 2024Takriban watu milioni 1 wanatarajiwa kupigia kura rasimu ya katiba, ambayo inapendekeza mabadiliko makubwa ambayo yanaweza kuzuia utawala wa nasaba na uhamisho wa madaraka, na inahitaji zaidi ya 50% ya kura ili kupitishwa.
Soma pia:Viongozi wa kijeshi wa Gabon watangaza kuandaa uchaguzi 2025
Rasimu hiyo ya katiba inaweka muhula wa miaka saba, unaoweza kurefushwa tu mara moja, badala ya katiba ya sasa inayoruhusu mhula wa miaka mitano bila ya kikomo. Pia inasema wanafamilia hawawezi kurithi urais na kuwania nafasi ya waziri mkuu.
Soma pia: Kiongozi wa kijeshi Gabon ateuwa wabunge wapya wa Bunge la Kitaifa
Mnamo 2023, wanajeshi wa Gabon walimpindua Rais wa muda mrefu Ali Bongo Ondimba na kumtangaza mkuu wa jeshi, Jenerali Brice Clotaire Oligui Nguema, kama rais wa kamati ya mpito kuongoza nchi.