Gaddafi apinga kutambuliwa kwa Baraza la Mpito la Waasi wa Libya
16 Julai 2011Matangazo
Kundi hilo la mashauriano kuhusu Libya, lilikutana jana mjini Istanbul Uturuki. Katika mkutano huo, lilitangaza kutambuliwa kwa baraza la waasi kama mwakilishi wa watu wa Libya na " serikali yenye mamlaka". Marekani imeungana na mataifa mengine makuu kuwatambua waasi wa Libya kama chombo halali cha uongozi nchini Libya.