1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaddafi asema Walibya wako tayari kufa kumlinda

1 Machi 2011

Matamshi yake yamekosolewa vikali na balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa akisema Gaddafi yuko mbali mno na ukweli halisi wa mambo nchini Libya

Gaddafi (kushoto)akisalimiana na Christiane Amanpour wa kituo cha habari cha ABC, mjini TripoliPicha: AP

Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amesisitiza kuwa raia wake wote wanampenda, hivyo kupuuza shinikizo la kimataifa linalozidi kumtaka aondoke madarakani na pengine akimbilie uhamishoni baada ya kuiongoza nchi hiyo kwa miongo minne. Katika mahojiano yake hapo jana na televisheni ya ABC, BBC na gazeti la The Times la jijini London, Gaddafi amesema Walibya wako tayari kufa kwa ajili ya kumlinda na kusisitiza hakuna anayempinga. Gaddafi amedai hakuna maandamano yoyote mabarabarani.

Matamshi ya kiongozi huyo yamelaaniwa vikali na balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan RicePicha: picture alliance / landov

Akizungumza katika ikulu ya Marekani mjini Washington, Bi Rice amesema matamashi hayo yanadhihirisha kwamba Gaddafi hafai kuongoza na amejitenga na ukweli halisi wa mambo. Wakati huo huo, Marekani imeanza jana kupeleka meli zake za kivita na ndege karibu na Libya. Marekani pia imezuilia mali za Libya za thamani ya dola bilioni 30 kumshinikiza Gaddafi aondoke madarakani.

Mwandishi: Josephat Charo

Mhariri: Aboubakar Liongo

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW