1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gambia yadai Myanmar ililenga kuangamiza jamii ya Warohingya

12 Januari 2026

Myanmar ilifanya mashambulizi ya kikatili dhidi ya jamii ya wachache wa Rohingya kwa lengo la kuiangamiza jamii hiyo, Gambia yasema.

Moto katika kambi ya Warohingya nchini Bangladesch
Moto katika kambi ya Warohingya wakimbizi wilaya ya Kutupalong Bangladesh Januari 7, 2024Picha: Shafiqur Rahman/AP/picture alliance

Waziri wa Sheria wa Gambia Dawda Jallow, ameiambia mahakama ya kimataifa ya Haki ICJ iliyoko The Hague Uholanzi Uholanzi siku ya Jumatatu, wakati wa kuanza kwa kesi ya mauaji ya kimbari.

Dawda amesema mashtaka yao si masuala ya falsafa za sheria bali ni masuala yanayowahusu watu halisi Warohingya waliolengwa kwa maangamizi.

Gambia ilifungua kesi kwa mara ya kwanza dhidi ya Myanmar, mnamo mwaka 2019 ikidai kuwa "operesheni ya kusafisha” iliyofanywa na jeshi la Myanmar mwaka 2017 ilikiuka Mkataba wa kuzuia Mauaji ya Kimbari wa mwaka 1948.

Uamuzi wa mwisho unaweza kuchukua miezi au hata miaka, na ingawa ICJ haina njia ya kutekeleza maamuzi yake, uamuzi unaounga mkono Gambia utaongeza shinikizo zaidi la kisiasa kwa Myanmar.

Myanmar ambayo kwa sasa ipo mikononi mwa utawala wa kijeshi imekanusha mashtaka dhidi yake.

Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, zimejiunga na kesi hiyo tangu wakati huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW