Mwanariadha Gatlin asubiri kupambana Beijing
17 Julai 2015Gatlin amesema kuimarika kwake katika riadha akiwa na umri wa miaka 33 kunahusikana na hatua ya kufungiwa nje ya mashindnao kwa misimu minne baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.
Wakati Mjamaica Usain Bolt akiendelea kusumbuliwa na tatizo la nyonga, Mmarekani huyo atashiriki katika mashindano ya ubingwa wa dunia mjini Beijing mwezi ujao akipigiwa upatu kushinda mbio za mita 100 na 200, baada ya kuweka muda bora wa kibinafsi wa 9.74 katika mita 100 mwezi Mei.
Gatlin amesema mwili wake unajihisi kama mtu wa miaka 27 na siyo 33 ambaye amekimbia miaka hiyo minne na kuchoka. Ameongoza kuwa inasikitisha kuwa hakushiriki mashindano, lakini aliweza kupumzika na kuwaona wapinzani wake wakiimarika.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters/AP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman