Gavana akamatwa kwa ufisadi Kenya
4 Julai 2018Matangazo
Gavana huyo, Sospeter Ojaamong, hakusema mengi kuhusu tuhuma taarifa hizo, lakini alikieleza kituo cha habari cha KTN nchini Kenya kwamba yeye ni mweupe kama pamba au theluji.
Mkuu wa kitengo cha uendesha mashtaka wa umma Noordin Haji amethibitisha kwamba maafisa 9 watasimamishwa kizimbani kuhusiana na wizi wa mamilioni ya fedha za umma.
Alisema mashitaka dhidi ya Gavana Ojaamong yatajumuisha matumizi mabaya ya ofisi yake, na hila ya kuiba mali ya umma.
Tuhuma za ufisadi dhidi ya gavana huyo zinatokana na zabuni katika mfumo wa ukusanyaji taka katika mji wa Busia ulio karibu na mpaka baina ya Kenya na Uganda.