1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Gavana wa Darfur awataka raia kubeba silaha na kupambana

28 Mei 2023

Gavana wa mkoa wa magharibi mwa Sudan ulioharibiwa kwa vita wa Darfur Mini Minawi amewahimiza raia kwenye eneo hilo "kubeba silaha" kujilinda na wale amewataja kuwa wahujumu wa taasisi za taifa.

Maelfu wamekimbia mapigano Sudan
Maelfu wamekimbia mapigano Sudan Picha: Blaise Dariustone/DW

Minawi ambaye ni kiongozi wa zamani wa kundi moja la waasi, amekaririwa akiliunga mkono jeshi la taifa linalopambana na kikosi cha wanamgambo wenye nguvu cha RSF tangu April 15.

Amesema raia wanapaswa kuchukua silaha kulinda mali zao dhidi ya watu wasiotaka usalama au haki za umma wa Sudan.

Mkoa anaongoza wa Darfur tayari umeshuhudia vita vya muda mrefu tangu mwaka 2003 na katika mapigano yanayoendelea sasa vifo na majeruhi vimeshuhudiwa pia kwenye eneo hilo.

Matamshi ya Minawi yanajiri katika wakati miito inaongeza ya kutaka majenerali wawili wanaowania madaraka nchini Sudan kurefusha muda wa kusitisha mapigano unaofikia tamati kesho Jumatatu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW