1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfghanistan

Gavana wa mkoa auawa katika shambulizi la kujitoa mhanga

6 Juni 2023

Kaimu gavana wa mkoa wa Badakhshan nchini Afghanistan ameuawa leo katika shambulizi la bomu la kujitoa mhanga. Shambulizi hilo limejiri miezi michache tu baada ya mkuu wa polisi wa mkoa huo kuuawa.

Afghanistan | Taliban-Kämpfer | Stadt Farah
Picha: Mohammad Asif Khan/AP/picture alliance

Kaimu gavana wa mkoa wa Badakhshannchini Afghanistan ameuawa leo katika shambulizi la bomu la kujitoa mhanga. Shambulizi hilo limejiri miezi michache tu baada ya mkuu wa polisi wa mkoa huo kuuawa katika shambulizi sawa na hilo lililodaiwa kufanywa na kundi la Dola la Kiislamu. Mlipuaji huyo aliliendesha gari lake lililojaa mabomu na kuligonga gari lililokuwa limembeba Nisar Ahmad Ahmadi ambaye alikuwa naibu gavana wa mkoa wa kaskazini wa Badakhshan kabla ya kupanda ngazi na kuwa kaimu gavana mwezi uliopita. Tukio hilo lilitokea katika mji mkuu wa mkoa huo Faizabad. Dereva wa gavana pia aliuawa na wengine sita kujeruhiwa kwenye shambulizi hilo ambalo hakuna aliyedai kuhusika mpaka sasa. Usalama umeimarishwa pakubwa tangu Taliban ilipokamata madaraka Agosti 2021, lakini kundi la IS bado ni kitisho.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW