Gavana wa Punjab auawa Pakistan
5 Januari 2011Matangazo
Kwa mujibu wa maafisa wa polisi, watu wengine watano pia walijeruhiwa katika shambulio hilo.
Gavana Salman Taseer, ni mhanga mashuhuri kabisa kuuawa katika mashambulio yaliyofululiza nchini Pakistan, tangu waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto kuuawa katika mwaka 2007.
Taseer, alikuwa mshirika wa Rais Asif Ali Zardari,ambae ni mjane wa Bhutto. Hivi karibuni, gavana huyo aliikosoa sheria inayohusika na adhabu ya kutolewa kwa vitendo vya kufuru. Waislamu wenye itikadi kali wameitetea sheria hiyo.