1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza: Hakuna usitishwaji wa mapigano licha ya makubaliano

10 Aprili 2026

Raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza wanaendelea kukabiliana na hali ya mashaka na matumaini yanayozidi kufifia, miezi 6 baada ya makubaliano dhaifu ya usitishaji mapigano kati ya Israel na Hamas kuanza kutekelezwa.

Gari linaloteketea baada ya shambulio la Israel Gaza.
Wapalestina wakishuhudia gari linalowaka moto kufuatia mashambulizi ya IsraelPicha: REUTERS

Makubaliano ya usitishwaji vita vilivyodumu kwa takriban miaka miwili yaliyosimamiwa na Marekani yalianza kutekelezwa mwenzi Oktoba mwaka uliopita.

Makubaliano hayo yalikuwa na masharti makuu ya kulinyang'anya silaha kundi la Hamas, kuongeza misaada ya kiutu, na kupeleka kikosi cha usalama cha kimataifa.

Wapalestina waliokuwa wameyakimbia makaazi yao pia walijawa na matumaini makubwa juu ya mipango ya ujenzi mpya kuanza mara moja.

Hata hivyo tangu makubaliano hayo ya usitishwaji mapigano yaanze kutekelezwa, jumla ya watu 738 wameuwawa na wengine 2,036 wakijeruhiwa kulingana na takwimu za hivi karibuni za Wizara ya Afya Gaza iliyochini ya Hamas, ambayo haitofautishi kati ya raia na wapiganaji wa Hamas.

Wakaazi wa Gaza wanasema licha ya makubaliano hayo bado wameendelea kushuhudia mateso, kama anavyoeleza Eyad Abu Dagga, mkaazi wa Gaza

"Hatujaona usitishaji wa mapigano hata kidogo katika miezi sita au saba iliyopita. Vita bado vinaendelea, na maisha bado ni magumu sana kama yalivyo. Kama raia, unaona kuna usitishaji wa mapigano?" alisema Eyad

Aliongeza kwamba  raia bado wameendelea kushuhudia mateso makubwa na kama jumuiya ya kimataifa imewasahau watu wa Palestina.

Misaada pia imeendelea kuingia kwa uchache kupitia mpaka mmoja unaodhibitiwa na Israel, hali inayodhihirisha changamoto pana zinazokabili juhudi za kurejesha amani, wakati mbinu ya Rais wa Marekani Donald Trump ikionekana kujikita kwenye kusitisha mashambulizi ya moja kwa moja na kuacha masuala mapana zaidi ya kisiasa yashughulikiwe baadaye, jambo linalozua mashaka iwapo mtindo huo unaweza kufanikiwa pia katika mzozo mpana zaidi unaohusisha Iran na eneo la Mashariki ya Kati kwa ujumla wake.

Je, Bodi ya Amani ya Trump imefikia wapi?

Bodi ya amani iliyoundwa na Rais Trump haijakutana tena hadi sasa ikisubiri majibu ya Hamas juu ya sharti la kusalimisha silaha, hatua ambayo inatajwa na wataalamu kuwa miongoni mwa mashart magumu zaidi na pengine inayozorotesha utekelezaji wa makubaliano hayo.

Wapalestina waanza kuhama kuelekea kusini mwa Gaza

01:25

This browser does not support the video element.

Afisa wa Marekani ambaye hakukata kutajwa jina, amesema Hamas haijawekewa muda maalum wa kujibu suala hilo akiongeza kuwa "uvumilivu hauwezi kuwa wa kudumu".

Kukosekana kwa ukomo wa muda kunaweza kudhoofisha shinikizo la kuchukua hatua. Wakati huo huo, juhudi za kidiplomasia zinaendelea kushughulikia migogoro inayoibuka katika maeneo mengine.

Mkurugenzi wa Bodi ya amani Nickolay Mladenov aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi uliopita kwamba, dunia haipaswi kupoteza mtazamo wake kuhusu Gaza wakati mizozo mingine inapoibuka.

Alisema chaguo lililopo Gaza ni "kurudi kwenye vita vipya au kuanza ukurasa mpya; kuendelea na hali iliyopo ama kuelekea mustakabali bora.” Akisisitiza kuwa, "hakuna chaguo la tatu.”

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW