1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza kutumbukia janga la kiafya - WHO

31 Oktoba 2023

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema kuwa janga la afya ya umma linakaribia kuzuka kwenye Ukanda wa Gaza kutokana na msongamano, uhamaji kwa watu wengi kwa wakati mmoja na uharibifu mkubwa wa miundombinu.

Wapalestina wakichota maji kwenye kambi ya wakimbizi ya Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza siku ya Jumatatu (Oktoba 30).
Wapalestina wakichota maji kwenye kambi ya wakimbizi ya Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza siku ya Jumatatu (Oktoba 30).Picha: Yasser Qudih/picture alliance/Xinhua News Agency

Msemaji wa WHO, Christian Lindmeier, alionya siku ya Jumanne (Oktoba 31) kuhusu hatari ya kuongezeka vifo vya raia visivyohusishwa moja kwa moja na mashambulizi ya Israel. 

Maafisa wa afya wa Gaza wanasema zaidi ya Wapalestina 8,300 wameshauawa tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi ya angani katika eneo hilo linalotawaliwa na Hamas.

Soma zaidi: WHO: Haiwezekani kuwahamisha wagonjwa Gaza

Israel inadai kuwa mashambulizi dhidi ya Gaza ni kulipiza kisasi yale ya Oktoba 7 yaliyofanywa na kundi la Hamas ambayo inasema yaliuwa watu 1,400 nchini Israel na kuwachukua mateka wengine zaidi ya 200.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW