GAZA: Machafuko yazuka huko Gaza
20 Julai 2005Matangazo
Machafuko yamezuka kati ya polisi wa Israel na waandamaji wanaoupinga mpango wa kuyaondoa makazi ya walowezi ya kiyahudi kutoka mkanda wa Gaza, uliopangwa kuanza mwezi ujao. Watu 20 wamekamatwa na polis katika lango la kijiji cha Kfar Maimon, yapata kilomita 15 kutoka Gaza.
Watu wasiopungua elfu 15 wamekusanyika katika eneo hilo wakitaka kuandamana katika makazi ya Gaza, licha ya hatua ya polisi kuyapiga marufuku maandamano hayo. Walinda usalama wamewazingira waandamanaji hao wasije wakaendelea na maandamano katika makazi hayo.